... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Alama za Vidole

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 139:13-18 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wantu, uliniunga tumboni mwa mama yangu. Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana, mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoumbwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla azijawa bado. Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; jinsi ilivyo kubwa jumla yake! Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; niamkapo nikali pamoja nawe.

Listen to the radio broadcast of

Alama za Vidole

Download audio file

Ni huzuni kujilinganisha na watu wengine halafu hatimaye tunajionakama hatufai.  Mimi sina akili, mimi sikimbii mbio, mimi sina sura nzuri, mimi sifanikishi mambo yangu kama fulani.  Ni huzuni kabisa.

Si kwamba kujilinganisha na wengine inaathiri hisia zetu tu, lakini pia inazuia juhudi zetu na uwezekano wetu; inazuia nia yetu ya asili  kutumia vipaji na vipawa vyetu tulivyopewa na Mungu kwa ajili ya manufaa ya wengine.  Inamkwamisha mtu asipate kuridhika kwamba ametimiza mapenzi ya Mungu kama aliyekusudia.  Huwa inatokea mara nyingi. 

Kwahiyo, ikifika hatua unajikuta kwenye shimo naamini kwamba Mungu anataka kuongea na wewe kupitia maneno ya Mtunga Zaburi aliyetoa dua hii: 

Zaburi 139:13-18  Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wantu, uliniunga tumboni mwa mama yangu.  Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.  Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana, mifupa yangu haikusitirika kwako, nilipoumbwa kwa siri, nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; macho yako yaliniona kabla sijakamilika; chuoni mwako ziliandikwa zote pia, siku zilizoamriwa kabla azijawa bado.  Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; jinsi ilivyo kubwa jumla yake!  Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; niamkapo nikali pamoja nawe. 

Rafiki yangu, wewe uliumbwa na mkono wa Mungu kwa njia ya kipekee, kwa njia inayopendeza mno kwa ajili ya siku alizoziandika kwa ajili yako.  Sikiliza, alikupa alama za vidole tofauti kabisa na watu wengine, ili uweze kuchapa alama ambazo hakuna mwingine awezaye kuchapa. Acha kujilinganisha na wengine. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.