... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hakuna Huduma Ndogo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 4:8-10 Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika; kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbli za Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Hakuna Huduma Ndogo


Download audio file

Ninachokitaka mimi ni kuwa muwazi mbele yako.  Muwazi na mkweli kabisa.  Kwasababu, na mimi ni mtu mdhaifu kama wewe, mtu ambaye hajakamilika.  Kwahiyo leo ni siku mojawapo ninayojitumia kama mfano mbaya.

Kazi yangu ya kila siku ni kuandaa ujumbe kama huu wa leo.  Ninaingia studio za redio na za TV kurekodi ujumbe, pia ninawajibika kuongoza huduma inayowafikia watu ma-milioni kwa kuwatangazia Habari Njema za Yesu.  Safi kabisa. 

Lakini kwa upande mwingine, kwa asili, mimi si mtu anayeweza kukaa na kusubiri mtu aje ili niongee naye habari za Yesu.  

Kwahiyo, kwangu mimi ni rahisi sana kujidanganya kwa kufikiri kule kuongea na mtu mmoja mmoja kuwa hakuna maana sana kwasababu ya majukumu yangu mengi niliyonayo.  Ngoja niwaachie wengine hiyo kazi.  Lakini mtazamo wangu sio sahihi! 

1 Petro 4:8-10  Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.  Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika; kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbli za Mungu. 

Kuwapenda watu kwa juhudi, kushiriki chakula nao, kuwaonyesha neema ya Mungu … ni kazi inayofanyika moja baada ya nyingine.  Wakati mwingine ni kazi ngumu inayosumbua sana,  Lakini machoni pa Mungu, ni muhimu sana! 

Kwahiyo, inatupasa sisi sote, wewe na mimi, kutafuta kuongea na watu, mmoja mmoja, kuwapenda sana, kushirikiana nao,hata kama wito wetu ni wa namna gani au kipawa tulicho nacho ni cha namna gani … kwa sababu kwa njia hii, ndio Mungu anayoitumia kubadilisha maisha ya watu – maisha yao na ya kwetu pia.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.