... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kilicho Muhimu Zaidi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

Listen to the radio broadcast of

Kilicho Muhimu Zaidi


Download audio file

Kupanga yaliyo kipaumbele sio rahisi pale unapokuwa na majukumu mengi.  Lazima utimize hiki na kile na kingine tena, kwahiyo ni pirika-pirika tu, mtu akizunguka kama kuku aliyekatwa kichwa.

Hivi karibuni mimi na mke wangu tulihama nyumba ili tuwe karibu na wajukuu wetu. Kweli tulifurahia pale tulipohamia. Lakini kama umeshawahi kuhama nyumba, unafahamu kwamba kuhama ni kazi inayochosha sana na mambo mengi.

Kuchambua vitu, kufunga mizigo, kuhakikisha malipo ya umeme huko mnakotoka na mnakoenda pia, kubadilisha anwani na kufahamisha walengwa, hayo yote bado ni kabla ya kuhama.  Halafu kuna kuhama na kufungua mizigo na kuamua kipi kiwekwe wapi – jamani, ni kazi ya wiki mbili inayochosha mno, kimwili na kimawazo pia. 

Katikati ya zoezi lile, niligundua kwamba kwa kusongwa hivyo, tulianza kukosa uvumilivu, tukitumia sauti kali na kushindwa kuchukuliana kwa jinsi isiyo ya kawaida. 

“Subiri kwanza,” niliwaza.  “Hii siyo sahihi.”  Na ni kweli, haikuwa sahihi!  Kusongwa na mambo mengi sio kibali cha kukosa adabu. 

Wakolosai 3:14  Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. 

Wakati mnahangaika na kusongwa hivyo, inabidi usimame kwanza na kutulia na kuvuta pumzi – kama tulivyofanya sisi wakati wa kuhama – ili mgundue upya kwamba kilicho muhimu zaidi katika maisha yetu mapya ni kupendana. 

Je! Tuko pamoja?  Hicho ndicho cha muhimu zaidi!  Kwa sababu upendo ndio kifungo cha ukamilifu.  

Kwahiyo haijalishi una majukumu kiasi gani, haijalishi umesongwa vipi, kumbuka hili:  kilicho muhimu kuliko vyote ni upendo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.