... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kubarikiwa Kupita Kiasi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:4,5 Namshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote.

Listen to the radio broadcast of

Kubarikiwa Kupita Kiasi


Download audio file

Sijui kama  unatarajia kupata baraka gani hivi karibuni kutoka kwenye mkono wa Mungu!, ulikuwa unamwomba nini?  Ni kipi cha kwanza katika orodha ya mahitaji yako, hmm?

Sisi sote tuna matamanio … na mara nyingi ni kama mchonyoto wa ndani kabisa hadi tusingeliweza kumwambia mwingine ila Mungu mwenyewe tu. Sasa leo tunataka kuongea kuhusu kile kitu unachotamani sana kukipata. 

1 Wakorintho 1:4,5  Namshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote. 

Mtu akiwa na shauku ya kupata kile kitu kimoja, ni rahisi kusahau kwamba, kufuatana na Neno la Mungu, tayari ameshabarikiwa katika kila jambo. Na ni kweli kabisa.  A.W. Tozer aliwahi kusema hivi: 

“Kuna wakati ninamwendea Mungu na kumwambia, ‘Mungu, hata kama hutajibu tena ombi langu lingine nikiishi hapa duniani, bado nitakuabudu maisha yangu yote kea yale ambayo tayari umeshanitendea.’  Mungu ameshaniwekea deni kubwa mno, kwahiyo hata ningeishi karne milioni, nisingeweza kulipa kwa yale yote ameyonitendea.”  Pia, Tozer aliongeza na hili: 

“Mungu hana haraka.  Hakuna ratiba inayombana katika utendaji wake.  Kujua hilo kutatuliza mioyo yetu na kupumzisha mawazo yetu … Labda inatakiwa imani safi zaidi kumtukuza Mungu kwa ajili ya baraka ambazo hazijaonekana kuliko zile ambazo tumeshazipokea.” 

Rafiki yangu, umebarikiwa sana sana.  Tulia sasa ukingoja baraka zingine zitakazokuja. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.