... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maisha Yenye Uwiano Mzuri

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mhubiri 4:5,6 Mpumbavu huikunja mikono yake, naye hula chakula chake mwenyewe; heri konzi moja pamoja na utulivu, kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo.

Listen to the radio broadcast of

Maisha Yenye Uwiano Mzuri


Download audio file

Kama mtu angekujia na kukupa ofa ya kuridhika, yaani kutoshelezeka na maisha yenye matunda na uwiano mzuri, je! Ungepokea ofa yake?  Nadhani wengi tungeipokea.

Ni kweli kabisa. Kwenye kiini cha mioyo yetu tunatamani kuwa na maisha yenye uwiano uletayo kuridhika.  Kwa upande mmoja, kutumia vipawa na vipaji vyetu kutimiza mambo mema.  Kwa upande mwingine, kuwa na muda wa kutosha kufurahia matunda ya kazi zetu. 

Siku hizi wanasema ni uwiano katika ya kazi na maisha.  Kwa hiyo acha niulize … Je! Uwiano wako kati ya kazi na uzima wako vinaendaje?  Wengine wanafanya kazi kupita kiasi wasipate burudani, wengine wanapenda burudani tu, wakiwa wavivu. 

Zamani mwaka wa 1965 kulikuwa na bendi maarufu ya Uingereza iitwayo The Rolling Stones, walikuwa na wimbo uliopendwa sana, usemao “Nimeshindwa Kuridhika”.  Ilidokeza tatizo la watu wengi walioshindwa kuwa na uwiano katika maisha yao. 

Sasa kwa kuwa teknolojia imetumeza siku hizi, labda maisha yetu yamezidi kukosa usawa mzuri tangu wakati ule.  Je! Kuna mapya katika hayo?  Wala.  Tumsikilize Mfalme Sulemani tena miaka 960 kabla ya Kristo: 

Mhubiri 4:5,6  Mpumbavu huikunja mikono yake, naye hula chakula chake mwenyewe; heri konzi moja pamoja na utulivu, kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo. 

Hapa hapa, baada ya miaka elfu tatu, ndipo Mungu anatuonyesha la kufanya kuhusu swala hili la uwiano wa kazi na maisha, swala ambalo limetuvurugu sana katika karne yetu ya 21. 

Sasa – ninataka kukuachia swali hili:  Je! Shauku yako ya kuzidi kupata mali imekuharibia maisha kiasi gani? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.