... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Makosa Wanaume Wanayofanya (2)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 6:1,2,4 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi ... Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Tarehe: Iju – 230818 Wanaume wengi sana wamehama kihisia kwenda

Listen to the radio broadcast of

Makosa Wanaume Wanayofanya (2)


Download audio file

Wanaume wengi sana wamehama kihisia kwenda mbali na familia zao – ni kama wamejiuzuru kwa nafasi ya kuwa mume na baba mzazi pia. Na hili ndilo kosa kubwa kuliko yote wanaume tunaweza kufanya kwa sababu bila mwanaume mcha Mungu, jamaa zinasambaratika kwa jumla.

Nadhani unajua inavyokuwa, Tunazamishwa sana kwenye shughuli zetu, tukikaa masaa mengi kazini, halafu tunafika nyumbani tumeishiwa nguvu kabisa.

Kwahiyo tunajitenga kwenye mawazo yetu ili tupate burudani kidogo, jambo ambalo si baya, lakini shida ni kwamba tunabaki humo humo.  Ndio maana wanaume wengi hawana sehemu tena kwenye mambo yanayopitika kwenye familia nyumbani kwao.

Tunaacha kufanya yale yanatakiwa tufanye kama wanaume.  Kupenda wake zetu, kulea watoto na kuwarudi, kuwatia moyo binti zetu wakianza kukua, kuwa kama mnara wenye nguvu kwa ajili ya vijana wetu wakikumbana na matatizo.

Ni huzuni kweli kusikiliza wanawake wengi wakikwambia kwamba waume zao wamekimbia majukumu yao kama kiongozi na kuacha kukabiliana na changamoto ndani ya familia.

Waefeso 6:1,2,4  Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.  Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi … Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

Enyi akina baba, ni wajibu wako kufundisha watoto wako kukuheshimu na kumheshimu mama yao.  Ni kazi ngumu.  Si kuwachokoza, bali ni kuwalea na kuwatia moyo katika hekima ya Mungu na upendo wake kwa kuwa kielelezo cha namna wanavyowapaswa kuishi.  Hii itaweka msingi imara wa maisha hata kwa ajili ya vizazi vitakavyofuata.  Hii inatakiwa mtu awe na juhudi kweli na kutumia nguvu za kutosha.  Inatakiwa mtu awajibike kihisia kwa kina kabisa.

Enyi waume, msijentenge, muajibike!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.