... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maneno Usingependa Kuyasikia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mariko 12:6,7 Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu.

Listen to the radio broadcast of

Maneno Usingependa Kuyasikia


Download audio file

Ukosoaji haupendezi, unatonesha kabisa, unaumiza, ni kweli, mimi sijakamilika lakini sipendi kusikia watu wengine wananisema. 

Kuna kozi ya uongozi ninaifatilia siku hizi na juzi nilimaliza zoezi linaloitwa, “uchunguzi wa duara” ambapo watu wote wanaonizunguka katika huduma yetu walipaswa kujaza fomu ya maswali yanayonihusu mimi, kuanzia kwenye bodi hadi watumishi wa ngazi ya chini.  Majibu yote yaliingizwa kwenye program ya komputa na ilinitolea ripoti ya karasa 30. 

Kweli, kulikuwa na mengi ya kunipongeza lakini kwa ababu sijakamilika, kuna mambo machache yaliniumiza. Sasa mtu afanyeje anaposoma ukosoaji huo?  Ama ataukataa kata kata (kama wengi wanvyofanya) au atautendea kazi na kujirekebisha, kitu ambacho ninajaribu kufanya  mimi sasa hivi. 

Yesu alitoa hadithi ya namna Israeli walivyokataa manabii wengi Mungu aliowatuma kwao.  Manabii wa uongo waliwaambia yale waliyotaka kusikia na kupelekea wananchi kuwapenda.  Lakini manabii wa kweli waliwaambia yale waliyopaswa kusikia … na watu waliwaua kwa kuwapiga kwa mawe.  Sasa.. 

Mariko 12:6,7  Basi alikuwa na mmoja bado, mwana mpendwa wake; huyu naye akamtuma kwao mwisho, akisema, Watamstahi mwanangu.  Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu. 

Yesu hawezi kukwambia kila wakati yale unayotaka kusikia – na ndio maana walimwua na yeye pia.  Hata hivyo, msikilize.  Kwa vyo vyote, tendea kazi yale akwambiayo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.