... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tembea Maili Moja

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 4:15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udahifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.

Listen to the radio broadcast of

Tembea Maili Moja


Download audio file

Bila shaka, umeshasikia msemo usemao, ukitaka kumuelewa mtu fulani, lazima utembee maili moja ukiwa umevaa vitatu vyake.  Hii ina maana kwamba, jiweke kwenye nafasi yake ili uweze kuwa na mtazamo kama wake.

Jana tulizungumza kuhusu namna watu wanavyohukumu watu wengine kwa haraka – Hatua ya kwanza ya kujuana na mtu vizuri ni kuahirisha hukumu.  Hatua ya pili ni kuchukua mtazamo wake, ina maana, kutembea maili moja ukiwa umevaa viatu vyake. 

Ukitafakari vizuri, kumbe, hilo ndilo jambo alilolifanya Yesu kwa ajili ya watu kama wewe na mimi. 

Waebrania 4:15  Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udahifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 

Ni kweli, kwa kuwa Mungu ni Mungu, tayari ameshajua tulivyo, kwanini tunajisikia hivi au vile, kwanini tunatenda hiki au kile?, ni kwa sababu anajua kila kitu; kila wakati.  Lakini, hata hivvyo, Yesu alipofanyika kuwa mwanadamu, Yesu aliamua kutembea maili moja akiwa amevaa viatu vyetu. 

Kwahiyo Mungu hajui tulivyo kama wanadamu kwa kuwa ni Mungu tu, lakini pia anatuelewa kwa sababu alifanyika kuwa mtu na yeye. 

Sisi hatujui vyote kila wakati kama yeye Mungu alivyo, lakini sisi pia tunaweza kuamua kujaribu kuangalia mambo kwa mtazamo wa mtu mwingine, kujaribu kuelewa anavyojaribiwa, kumthamini akipitia vipindi vigumu. 

Kufanya hivyo kunasaidia nini?  Kunafungua mlango ili tuone ubinadamu wake ili tuweze kuelewa mapambano aliyo nayo, tuweze pia kuwa na huruma kwake. 

Yesu, kwa kweli alitoa mfano unaotikisa.  Tembea maili moja ukiwa umevaa viatu vyake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.