... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Alikuchagua kwa Kusudi Maalum

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 1:3,4 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.

Listen to the radio broadcast of

Alikuchagua kwa Kusudi Maalum


Download audio file

Je! Unamwamini Yesu?, unaamini kwamba alikufa ili alipe deni la dhambi zako?, akafufuka ili akupe maisha tele, maisha mapya pamoja na uzima wa milele?  Kama jibu lako ni ndiyo, basi nina habari njema kwa ajili yako leo.  Habari njema kabisa.

Jana tuliongea habari ya kweli kwamba mtu akimwamini Yesu, tayari atakuwa ameshabarikiwa baraka za kiroho ndani ya Yesu.  Maneno mawili makuu ya kuzingatia ni “tayari” na “kila”. 

Lakini tupige hatua nyingine kwasababu kuna lengo la baraka, yaani lengo la mafuriko ya neema ya Mungu kwetu.  

Waefeso 1:3,4  Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 

Jaribu kutafakari kwanza ukitulia.  Kabla viumbe havijakuwepo, tayari ulikuwa umechaguliwa katika Kristo.  Ndio kabisa!  Wewe ulijulikana hivyo moyoni mwa Mungu.  Tena si kwamba ulikusudiwa upate baraka tu, kana kwamba ingetosha. 

Lakini pia, alikusudia uwe mtakatifu, bila hatia mbele zake katika pendo.  Ina maana, damu ya Kristo imekuosha, imekutakasa kama thelugi inayoshuka kutoka mawinguni, dhambi zako zote zikioshwa kabisa kupitia yale Yesu aliyokutendea. 

Sasa hatua inayofuata katika baraka hizi za ajabu, ukiwa njiani kuishi milele huko, ni mwenendo wako safarini, kuwa safi, bila hatia.  Sehemu hii ni muhimu kwa sababu ndivyo ulivyokusudiwa uwe ndani ya Kristo.  Kwa hiyo, kama unataka mwaka huu mpya unaokuja uwe bora kuliko mwaka uliopita, ishi sawa sawa na kusudi la wito wako.  Ishi maisha matakatifu, usiwe na hatia.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.