... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Amani ya Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 4:6,7 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.

Listen to the radio broadcast of

Amani ya Mungu


Download audio file

Tangu mwanzo, fadhaa imekuwa ugonjwa sugu ambao umenyanganya uzima watu ma-miliyoni.  Halafu katika ulimwengu wetu wa kisasa, kasi ya teknolojia na mtandao imesababisha watu kufadhaika na kusumbuka zaidi ikiongeza madhara katika binadamu.

Kwa hiyo, niambie, ni kipi ambacho kinakufadhaisha sasa hivi?  Ni kipi kinachokutafuna kwa ndani, kikikuangaisha, na kukukosesha usingizi?  Ni kweli, hatuna budi kukutana na mawimbi maishani.  Pia, ni kawaidi mwanadamu kuwa na mwitikio wa kufadhaika akiwa shidani. 

Lakini kwa yule aliyeweka tumaini lake kwa Yesu, hakuna sababu ya kuendelea kuishi daima katika hali ya mafadhaiko.  Akiwa gerezani, akisubiri hukumu ya kifo, Mtume Paulo aliandika hivi: 

Wafilipi 4:6,7  Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.  Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. 

Tujisumbue kwa neno gani?  Hamna, tusijisumbue kwa neno lo lote! 

Sasa mtu atawezaje kushika amani ya Mungu katika kipindi kigumu?  Ni kwa njia ya kusali katika mazingira yoyote, akimwaga nafsi yake mbele zake – si kwa manung’uniko, bali kwa kushukuru – akimwambia Mungu mawazo yake na haja zake. 

Pia, hii ni sehemu inayonigusa zaidi; ni kwamba, tukifuata ushauri huu, basi amani ya Mungu, amani ipitayo akili za wanadamu, amani isiyotazamiwa katika mazingira yetu magumu, si kwamba itajaza mioyo yetu tu – bali italinda mioyo yetu pia, ili mtu yeyote akiwemo Shetani, asiweze kutunyang’anya amani tuliyopewa na Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. 

Rafiki yangu, nisikilize vizuri.  Hii ni ahadi ya Mungu kwako leo, tena ni ahadi inayoaminika kabisa, iliyofanya kazi kwa watu wasiohesabika.  Leo, amani hii ipitayo akili, inaweza kuwa yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.