... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Bahati Nzuri au Bahati Mbaya?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Danieli 4:34,35 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia, nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?

Listen to the radio broadcast of

Bahati Nzuri au Bahati Mbaya?

Download audio file

Kila asubuhi, mama yangu mzazi alipenda kusoma uaguzi wa nyota kwenye gazeti. Ni jambo ambalo huwa tunalijadili mara nyingi tunapokuwa tunakunywa chai asubuhi.  Kwani kuna ubaya wowote katika hilo?

Kwani, Kuna ubaya wowote kusoma mambo yahusuyo nyota?  Jibu ni kwamba ni chukizo kwa Mungu kwasababu kunatufanya tuweke imani yetu katika kitu kingine tofauti na yeye. 

Pia, maswala ya bahati, nasibu,.. na mifumo mingine mingi ambayo inaonekana kwamba haidhuru lakini mizizi yake imetoka kwenye imani zingine zinazovuta watu waweke tumaini lao pengine na si kwa Mungu mwenyewe. 

Nebukadreza alikuwa mfalme wa Babeli.  Alikuwa ametafuta waganga, wapiga ramli, watabiri.  Pia alijenga sanamu kubwa ya dhahabu kwa sura yake akilazimisha watu wote waiinamie na kuiabudu.  Lakini baada ya kukutana na Danieli na rafiki zake kimiujiza, maisha yake yalibadilika mno hadi akafikia maamuzi haya: 

Danieli 4:34,35  Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia, nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly