... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Endelea, Usichoke

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.

Listen to the radio broadcast of

Endelea, Usichoke


Download audio file

Uwepo wa dhambi ni ukweli usioepukika.  Najua kama siku hizi watu wengi hawapendi kusikia habari za dhambi, lakini tangu lini maoni ya wengi yamekuwa kipimo cha kujua ukweli?  Hakika, dhambi ni ukweli usioepukika.

Ni kama mtu anataka kujirekebisha, kutengeneza maisha yake na mahusiano aliyo nayo na watu wengine, kuwa mtu bora kuliko jana, ni lazima akabiliane na hali halisi ya mambo.  Kuna dhambi inayoibuka katika fikra zetu hata katika matendo yetu.  Labda kwako itadhihirika tofauti na mimi, lakini kila mtu atapambana na zake. 

Kuna wakati tunajikwaa na kurudia kujikwa tena na tena huku tukitenda dhambi ile ile. Kuna wakati tunaanguka mpaka chini kabisa. Kuna wakati inafikia mahali mtu anajiona  kama hawezi kabisa kuwa na ushindi juu ya dhambi ile. 

Lakini kufikia hitimisho kama hiyo inatokana na mtu kusahau kwamba Mungu yuko pamoja nasi katika mapambano yote na atatufikisha ng’ambo.  Tunawezaje kuwa na uhakika huo?  Sikiliza: 

Wafilipi 1:6  Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu. 

Wewe na mimi tunaweza kuwa na uhakika wa ahadi hiyo, kwasababu Mungu anatenda kazi ndani yetu.  John Newton aliyeishi karne ya 18, tena hapo mwanzoni akiwa mfanya biashara wa watumwa alieleza hivi: 

Sijawa mtu anayestahili kuwa, pia sijawa mtu niliyetaka niwe, lakini kwa neema ya Mungu, mimi si tena mtu yule niliyekuwa zamani. 

Kumbukumbu:  Usimsahau Mungu katika mahesabu yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.