... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Furahia Mambo Bila Kunung’unika

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 2:14,15 Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu.

Kwa asilimia kubwa, mambo ya muhimu katika maisha yako yanaendelea shwari mahusiano na watu wengine, afya yako, uchumi lakini kuna kile kitu kimoja ambacho bado kinakusumbua sana.

Tunataka kulalamika na kunung’unikia kile kitu kimoja kana kwamba hatuoni mambo mengine yote ambayo yanaendelea vizuri maishani mwetu.  Kwa nini tunafanya hivyo?  Nafikiri tabia ya mwanadamu ndivyo ilivyo. 

Kwa hiyo, tunaweza kushtuka tukimwangalia Yesu na kugundua kwamba hakuwahi kunung’unika hata siku moja. Je!  Umeshawahi kusoma maneno ya manung’uniko yaliyo toa mdomoni mwake hata mara moja?  Hamna. 

Hata wakati ule aliosalitiwa na Yuda na kuhukumiwa, akapigwa na kudhihakiwa na hatimaye kugongelewa na misumari kwenye msalaba.  Hakutamka hata neno moja la manung’uniko!  

Wafilipi 2:14,15  Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu. 

Kwa mistari hiyo, Mungu anatuambia tufanye mambo mangapi pasipo manung’uniko wala mashindano?  Mambo yote!  Kwa nini sasa tutende yote bila manung’uniko?  Tupate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila. 

leo hii, tupate maono kwa pamoja.  Haijalishi mambo yangekuwia vigumu kiasi gani, acha kulalamika, acha kunung’unika, acha mashindano ya maneno … Songa mbele tuu… 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly