Hazina Njema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Magonjwa ya moyo na ya misipa ya damu – yaani presha, mshituko wa moyo na strok – yanasababisha theluthi ya vifo katika wanadamu. Yataua watu 51,000 duniani leo, na kesho yataua idadi ile ile na kesho kutwa hivyo hivyo na kuendela kila siku ya mwaka.
Magonjwa hayo kwa sehemu kubwa, yametokana na utamaduni ya magharibi kuenea duniani kote; yaani matumizi ya chakula kitokacho kiwandani pamoja na kupungua kwa kazi zinazohitaji nguvu za kimwili. Unajua, miaka mia iliyopita, magonjwa hayo hayakuwepo kabisa.
kama tungebadilisha na kutumia chakula kilicho freshi na kizima – chakula kinachoonekana kama kilivyo machoni mwa mtu – matunda, mboga, nyama na samaki badala ya chakula kilichowekwa ndani ya kopo, nadhani tungeweza kuokoa maisha ya watu ma-miliyoni.
Inahuzunisha kweli. Lakini kuna aina ingine ya magonjwa ya moyo inayohuzunisha pia. Ni ugonjwa ambao umeathiri maisha ya wanadamu tangu siku ile Adamu na Hawa walichuma tunda kwenye mti ule mmoja uliokatazwa bustanini. Yesu alieleza hivi:
Luka 6:45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Kwa hiyo, tuulize, Je! Moyo wako una hali gani? Labda mwenendo wako umebadilishwa kutoka kwenye mema ambayo Mungu anatamani kujaza moyoni mwako, na badala yake ukaingiza maovu yaliyotengenezwa katika viwanda vya ulimwengu huufanya maboresho leo hi hii … Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.