... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ijue Thamani Yako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 12:6,7 Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu. Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi.

Listen to the radio broadcast of

Ijue Thamani Yako


Download audio file

Je! Umewahi kujisikia kama wewe ni takataka; kana kwamba ulimwengu umekutafuna na kukutema?!  Wengine wote wanafurahi, wamestawi, wanaendelea na maisha vizuri, lakini wewe … umeshatupwa kwenye jalala.

Si mpaka msiba mkubwa ukukute ndo ukumbuke.  Hali ya kujisikia hufai inaweza kututafuna sisi sote, kwa kuwatazama tu wale wengine waliofaulu kwenye maisha yao. 

Wanaishi maisha yanayotikisa wakati sisi tunabaki tukijiuliza kama lolote tunalolifanya lingeweza kuwa na msaada wowote kwa watu wengine.  Ni wengi wanajiona wanyonge. 

Au labda wewe umeshazeheka.  Unaangalia vijana wa siku hizi – wanaoonekana kuwa chapu sana, wazoefu wa teknolojia ya kisasa – na inaonekana wamekushinda kabisa. 

Sasa kama unatatizwa na hali kama hiyo, sikiliza alichokisema Yesu kuhusu mada iyo hiyo: 

Luka 12:6,7  Je!  Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili?  Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.  Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote.  Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi. 

Ni mfano wa kawaida wa kila siku lakini unamtikisa mtu.  Huyu ni Yesu mwenyewe akiongea na wewe moja kwa moja.  Isitoshe, hakuongea tu bali alikubali kupelekwa msalabani na kugongomewa misumari kwa ajili yako, ili uweze kuishi naye milele.  Kwa hiyo, Usiogope basi, bora wewe kuliko mashomoro wengi.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.