... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupita Maisha Haya ya Hapa Duniani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 15:17-19 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu tumemetumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.

Listen to the radio broadcast of

Kupita Maisha Haya ya Hapa Duniani


Download audio file

Tangu miaka 2000 iliyopita, watu ma-bilioni wameamini habari za kifo cha Yesu Kristo na ufufuko wake.  Ni rahisi kuamini habari ya kifo.  Lakini habari ya ufufuko, je!  Ni rahisi kuiamini?  Nijibu sasa!

Sasa, wale watu ma-bilioni, walikuwa sahihi kwa kutegemea kwamba kifo cha Yesu kiliweza kulipa deni la dhambi zao na kuamini pia kwamba ufufuko wake unawaokoa na kuwapa karama ya uzima wa milele!? 

Kwa mtazamo wa kawaida wa kibinadamu … inaonekana kwama wale watu wamejidanganya.  Lakini nisikilize vizuri.  Kifo na ufufuko wa Yesu vinaenda sambamba.  Yaani huwezi kutenganisha matukio hayo mawili.  Ni eidha mtu aweke tumaini lake kwa Yesu kwa matukio hayo yote mawili au aache yote.  Hayo ndiyo aliyoyasema Mtume Paulo mnamo mwaka wa 60 baada ya Kristo: 

1 Wakorintho 15:17-19  Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.  Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.  Kama katika maisha haya tu tumemetumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. 

Kauli ambayo ndio msingi wa maelezo ya Ukristo – hata hitimisho lake – linasimamia kwenye ukweli kwamba, Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu kweli kweli.  Hatutakiwi tumwamini Yesu ili tupate maisha bora hapa duniani tu – hata kama maisha mapya ni mmojawapo wa mafao – lakini hasa ni kwamba tupate kuishi naye milele daima, hii ndio fursa kubwa tunayoipata kutoka kwenye ushindi wa kaburi lake. 

Ni kweli, umtegemee Yesu ili upate uzima tele, maisha yaliyo bora hapa duniani.  Lakini hii ni kama tone tu kwenye maji ya bahari ukilinganisha na uzima wako wa kuishi naye milele na milele.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.