... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Imani Yote Uliyo Nayo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 17:19,20 Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.

Listen to the radio broadcast of

Imani Yote Uliyo Nayo


Download audio file

Sijui kama umewahi kujisikia hivi, “Mimi sina imani ya kutosha ya kunipitisha katika magumu haya?”  Wakati unahitaji imani zaidi, ukiwa jangwani, ndipo unakuta imani imekukimbia. Hali hii imewatokea wengi, sio wewe tu! 

Mimi kama mtu aliyefaulu kupata digrii mbili za hesabu, naweza kukwambia kwa uhakika kwamba ni siku elfu kumi na siku sita,  tangu tarehe 15 Oktoba, 1995 nilipomwendea Yesu na kumwomba anisamehe, nakukabidhi maisha yangu miguuni kwake. 

Kama unavyoweza kufikiria, kumekuwa na milima na mabonde tangu nilipoamini.  Na kama wewe au hata mimi kuna wakati nimejikuta mabondeni kwenye hatari na giza nene, nilihisi kwamba imani yangu imetoweka. Kama nilivyosema, hauko peke yako.  Kumbe, kulikuwa na watu wengine wanaojulikana wakiwa wamepatwa na hali hiyo: 

Mathayo 17:19,20  Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa?  Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu.  Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. 

Juzi niliona picha ya punje ya haradali, mbegu ndogo sana – yaani mbegu iliyojulikana wakati wa Yesu kuwa  ni mbegu ndogo kuliko zote – kalikuwa kwenye ncha ya kidole cha mtu.  Picha ile ilikuwa na kichwa cha habari:  Ange!  Nina punje ya haradali, na sitasita kuitumia!.

Kama kiasi hicho cha imani ndicho ulicho nacho, basi itakutosha kabisa kwa kila tatizo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly