... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kabla ya Majira Yoyote

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yohana 1:1-5 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

Listen to the radio broadcast of

Kabla ya Majira Yoyote


Download audio file

Tayari, baada ya siku tatu itakuwa Krismasi.  Je!  Umechangamka?  Hmm!  Watoto bila shaka wanatarajia zawadi kwa shangwe, lakini kwa watu wazima wengi, wanaona Krismasi ingine ni kawaida tu.

Hatuna uhakika kwamba Yesu alizaliwa mwisho wa mwezi wa Desemba.  Wachungaji, sidhani wangekuwa wanachunga kondoo kondeni usiku majira yale ya baridi sana nchini Israeli, sidhani.

Ila dhana ya kumtuma Yesu ulimwenguni kutuokoa na dhambi zetu – yaani uasi wetu dhidi ya Mungu, na maovu yale yote sisi na wengine wote waliyoyafanya kwa kujiharibia na kuharibu ulimwengu wetu na kuleta maumivu na mateso mengi – ni dhana ilianzia kabla ya majira yote, kabla ya uumbaji tangu milele zote.  Daima dhana hiyo ilikuwa katika fikra zake na moyo wake Mungu.

Yohana 1:1-5  Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.  Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.  Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.  Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.  Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

Mtume Yohana anamwita Yesu kuwa “Neno” – yaani Mungu akiongea nasi.  Pia, nadhani unakumbuka pale Mwanzo sura ya kwanza neno la kwanza alilotamka Mungu katika kuumba?  Mungu alisema, Iwe nuru!  Ikawa nuru.

Yesu alikuja awe nuru ya ulimwengu huu, ulimwengu unaomoishi wewe.  Alikuja kuang’aa nuru maishani mwako.  Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.  Hii ndiyo maana ya Krismasi.  Pia …  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy