... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuacha Kumbukumbu Isiyoondoka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 37:37,38 Umwangalie sana mtu mkamilifu, umtazame mtu mnyofu, maana mwisho wake mtu huyo ni amani. Wakosaji wataangamizwa pamoja, wasio haki mwisho wao wataharibiwa.

Niko kwenye kundi la wafanyakazi kwa takribani miaka hamsini, kuna watu wachache sana bado wako kwenye kumbukumbu zangu ambao ninaseweza kusema kwamba ni wastaarabu kabisa kabisa. 

Ndivyo ilivyo, tunakutana na watu wengi sana njiani, lakini ni mara chache kukutana na mtu anayegusa moyo na kuleta mabadiliko endelevu ndani ya maisha yako.  Mimi nimeshasaidiwa na Jenerali, mchungaji, mshauri, meneja wa hoteli, Haijalishi mtu anafanya kazi gani, kuna kitu mtu anaweza kufanya.

Zaburi 37:37,38  Umwangalie sana mtu mkamilifu, umtazame mtu mnyofu, maana mwisho wake mtu huyo ni amani.  Wakosaji wataangamizwa pamoja, wasio haki mwisho wao wataharibiwa. 

Uwe mkamilifu na mnyofu, Ukisikia agizo hilo unawaza nini?  Tuwe wawazi, ni agizo linalotoka kwa Mungu mwenyewe, Kama mtu ni mstaarabu, muwazi, anawajibika, anajali watu wengine kutoka moyoni, huyo basi ni mtu anayefuata amani kwa hekima zote, anayeweza kushinda bila kufanya vita. 

Halafu watu wanaoishi hivyo, watu wanaopenda kwa upendo huo, watakuwa na uzao mkubwa, si watoto waliozaa tu, bali hata katikati ya watu waliotikiswa na wema wao.  Lakini wale wanaoishi tofauti hawatakumbukwa. 

Uwe mkamilifu na mnyofu.  Uwe mtu mwenye sifa hizo.  Acha kumbukumbu nzuri na endelevu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.