Kudai Haki Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Kwa maisha yako ya sasa hivi, pamoja na shughuli ulizo nazo, ni yapi ambayo unaamini kuwa ni haki yako? Yaani haki zile za msingi za kibinadamu.
Je! Ninani awezaye kupinga haki za uhuru wa fikra, uhuru wa kunena na kukusanyika pamoja, uhuru wa ibada? Lakini siku hizi wapinzani wapo, wanaofikiri imani yako ni takataka, wanataka kulazimisha ili tukubaliane nao, hao ndio wanaopinga uhuru wetu.
Hii ndiyo hali ya ulimwengu wetu leo; watu wanadai kwamba maono yao, imani yao, mienendo yao, vyote vikubaliwe na kupongezwa na watu wote kwa kusisitiza hali ya kuwa anuwai.
Unaona, kama hatukubaliani kwa jambo fulani, nikilazimisha ukubaliane nami na wewe hivyo hivyo, usisitize nikubaliane na wewe … tutaenda wapi jamani?
Nilisoma jambo la busara juzi: kusisitiza upewe haki zako bila kukubali wajibu ulio nao si uhuru, bali ni tabia ya ujana tu.
Kama wewe ni mtu unaemwamini Yesu wajibu wako ni upi?
Yohana 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
Kama vile Mtume Paulo alivyoandika, Yesu alitoa uhai wake kwa ajili yetu wakati tulikuwa bado katika dhambi zetu.
Mimi ninona haki moja tu niliyonayo kama mfuasi wa Yesu ni kuchukua msalaba wangu na kumfuata. Na itanigharimu sana!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.