... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuhurumiana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 3:8,9 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

Listen to the radio broadcast of

Kuhurumiana


Download audio file

Sijui kama umewahi kula kipande kigumu cha nyama? Wanasema kwamba kinasaidia kiafya na kuna wawengine wanaweza kulipa fedha nyingi ili kukinunua. Lakini kama ni ngumu sana baada ya kupikwa, ni bora ukiache tu. 

Kuna vitu vingine ni vizuri vikiwa vigumu.  Mfano, nyayo za viatu vyako.  Lazima ziwe ngumu.  Lakini kuna vitu vingine maishani ambavyo tunapendelea visiwe vigumu, viwe laini. 

Tuchukue mfano mwingine wa moyo wa mtu. Tunapenda mtazamo wa mtu mwingine pamoja na kuwa mtu imara, awe mpole, mwenye huruma, mtu anayejali watu wengine. 

Mtume Petro alikuwa anawaandikia watu waliokuwa wanateswa vibaya kwa sababu ya imani yao ndani ya Kristo.  Katika mazingira kama hayo, wakati mtu amebanwa vibaya, ni rahisi awe na moyo mgumu ili apambane na dhiki; lakini hatari ni kwamba, anaweza kuanza kuwa na moyo mgumu dhidi ya watu wote wanaomzunguka. 

1 Petro 3:8,9  Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitivu, wanyenyekevu; watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. 

Je!, unaposongwa na matatizo, muitikio wako ni upi? Ni swali ambalo yatupasa kujiuliza sisi sote.  Kwasababu, Mungu kamwe hataki moyo wako ufanywe mgumu, bali anataka uwe na moyo mwororo.  Uwe msikivu, uwapende watu wanaokuzunguka. Uwe mnyenyekevu, usirudishe ubaya kwa ubaya wala laumu kwa laumu.  Bali uwe mwenye kubariki. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly