... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumpendeza Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 19:14 Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Kumpendeza Mungu


Download audio file

Labda wewe ni mtu anayetaka kumpendeza Mungu, lakini (nadhani umeshagundua hili) si jambo rahisi kila wakati.  Kwahiyo … mtu atafanyaje ili aweke msingi imara ya kufaulu na kuishi maisha yanayompendeza Mungu kweli kweli?

Mara nyingi tabia yetu mbaya, dhambi zetu vinatutenganisha na hali halisi ya mambo.  Ukianguka ndani ya mtego ule ule tena … inaonekana kwamba ni wewe peke yako.  Tuwe na maono siku ya leo.  Si wewe tu peke yako.

Hayo yanamtokea kila mtu anayekusudia kumfuata Yesu.  Yalimtokea na Mtume Paulo aliyeandika hivi – Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. (Warumi 7:15)

Swali lililopo, je!  Tufanyeje kubadili hali hiyo?  Tunawezaje kuacha kutenda uovu tunaouchukia na kuanza kutenda mema tuyapendayo?  kweli, lazima tuanze ndani kabisa kwenye kiini cha mioyo yetu. 

Zaburi 19:14  Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA. 

Mambo unayoyatafakari ndiyo hatimaye utakayotamka na kutenda.  Kwa mstari huu, mtunga zaburi anaonyesha shauku kubwa aliyokuwa nayo kwa Mungu, kwamba mawazo yake na maneno yake yampendeze Bwana wake ambaye ni Mwamba wake na Mkombozi wake. 

Je! Ni mara ngapi unaomba dua kama hiyo?  Ni mara ngapi unamwendea Mungu na kumwomba kwa nguvu zako zote kwamba maneno yako na mawazo yako yapate kibali mbele zake? 

Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA.  

Umkaribishe Mungu akusaidie kuishi maisha ya utaua. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.