... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumtumainia Bwana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 27:13,14 Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA katika nchi ya walio hai. Umngoje BWANA, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.

Listen to the radio broadcast of

Kumtumainia Bwana


Download audio file

Sio rahisi kutenganisha kati ya kumtumainia mtu kikawaida na kumtegemea kupita kiasi. Lakini acha nikuulize swali: Je! Mtu anaweza kumtumainia Mungu au kumtegemea kupita kiasi?

Mimi nahisi kwamba mara nyingi tunaelekea kukosa kumtumaini Mungu pale  tunapokumbana na changamoto za mazingira magumu. Matumaini yetu huwa yanayumba pale tunapokabiliana na adui. Ebu, jaribu kufikiria ilivyokuwa pale ulipokuwa kwenye kipindi kigumu. Kwa kutumia kipimo cha sufuri hadi kumi, je! Matumaini yako ndani ya Mungu yalikfika kiwango gani?

Kinachoweza kutusaidia kuzidi kumtumainia Mungu ni kile kipindi tunapopitia mazingira yenye changamoto tena na tena, kwasababu kila wakati tunapopitia mazingira hayo tunaweza kuangalia nyuma na kuona namna Mungu alivyotuokoa. 

Labda ndio maana Mfalme Daudi alikuwa na moyo mkuu kwa kumtegema Mungu kabisa – alikuwa ameshashuhudia namna Mungu alivyomuokoa na hatari ya kifo. 

Zaburi 27:13,14  Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA katika nchi ya walio hai.  Umngoje BWANA, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA. 

Je! Unafikiri Daudi kipimo chake cha kumtegema Mungu kilikuwa kikubwa zaidi?  WalaNi kwa kuwa alishazoea kupitia uchungu wa vipindi vigumu kwamba Mungu ni mwaminifu; kwamba Mungu ni wa kutegemea. Halafu ushauri wake kwetu wewe na mimi, ni kwamba, wakati wa shida, alijifunza kumgonjea Bwana 

Umngoje BWANA, uwe hodari, upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.  Umngoje ukitumaini, ukitazamia kwamba Mungu atakuonekania na kukushindia adui wanapokushambulia.  Umngoje Bwana! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly