... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupendwa Hata Kama Hatustahili

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Listen to the radio broadcast of

Kupendwa Hata Kama Hatustahili


Download audio file

Kuna watu wanaweza kuchukizwa nasi kwa sababu zisizoeleweka au hata kinyume cha haki kabisa.  Ni kweli, hata mtu afanyeje hawezi kupendeza watu wote. Lakini hata hivyo, kuchukiwa kunatuumiza kwa sababu sisi sote tunapenda kupendwa.

Ni ukweli usioepukika  unaoumiza kuona watu baadhi hawakupendi.  Hata kukuchukia.  Kuna wakati wako sahihi, pengine inaeleweka ni kwanini hawakupendi na kuna wakati ni uonevu mtupu tu. 

Kwa haraka haraka ningeweza kutaja majina ya watu watano au sita ambao hawanipendi kabisa. Bila shaka, wako wengine wengi.  Ndio, kuna wakati mwenendo wangu kupitia kwa miaka mingi ulisababisha wanichukie, inaeleweka kwa sehemu lakini wakati mwingine ninasingiziwa tu. 

Sasa mtu atafanyaje?  Wewe, unafanyaje wakati unachukiwa?  Je!  Unaacha tu ukiendelea kuumia ndani au unakabiliana na hali kama hiyo?  Ukiamua kukabiliana nayo, je!  Unatumia njia gani?. Mtume Paulo aliandika hivi: 

Warumi 5:8  Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 

Sijui wewe, lakini mimi binafsi, nikitulia na kuanza kutafakari maneno hayo, kwa kweli ninashangaa mno. Mungu alikuwa na sababu zote za kunichukia, naam hata sasa, Nadhani hata wewe, tukizingatia yale yote tumeyatenda maishani.  Lakini badala ya kutuchukia, kwa kutumia tendo kuu la upendo kuliko yote, alimtuma Yesu kufa na kulipa deni la dhambi zetu. 

Mwanatheolojia  kutoka Marekani aitwaye R.C. Sproul alieleza hivi:  “Wakati najisikia kwamba nimeonewa na kuchukiwa, ninajaribu kukumbuka jinsi ninavyopendwa bila kustahili hata kidogo.” 

Hii ndiyo njia ya kukabiliana na hali ya watu kukuchukia! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.