... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kurudia Tena na Tena

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:1 Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Kurudia Tena na Tena


Download audio file

Imewahi kunitokea maishani mwangu (bila shaka na hata kwako pia) furaha ya Bwana, ni kama imetoweka. Yesu alisema na akafanya kama alivyosema ili tuwe na furaha tele.   

Hakuna jambo lenyekutuwezesha kama furaha ya Bwana.  Ndio, mtu anaweza kuwa na furaha kiasi, kama mwitikio wa hisia zake kulingana na mazingira yake.  Mfano, mambo yakienda sawa mara nyingi huwa tunafurahi; na yasipoenda sawa, tunahuzunika.  Lakini furaha ya Bwana ni kama chemchemi ya maji ya uzima unayobubujika kutoka ndani, si kwa sababu tumeitengeneza sisi wenyewe, lakini ni kwasababu kila mtu anayemwamini Yesu, mito ya maji ya uzima lazima itoke kwenye kiini cha nafsi yake, amina? 

Nikikwambia hayo mimi, labda inaweza kukutikisa kidogo tu.  Lakini Mungu mwenyewe anakwambia kupitia Neno lake, Roho Mtakatifu atakukumbusha na kukuburudisha kwa namna maneno ya binadamu wenzako hayawezi kufanya hata siku moja. 

Wafilipi 3:1 Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana.  Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi

Mimi pia ninajisikia kama vile Mtume Paulo katika mistari hiyo.  Mara nyingi narudia mada hii nikikwambia habari ya furaha ya Bwana ili uwe tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha haya. 

Si kwamba hakuna mada zingine ambazo tungejadili leo!?, hapana, ni kwamba, furaha ya Bwana ni muhimu sana, yaani ni ya ajabu … kwa hiyo hainiudhi kurudia-rudia 

Furaha ya Bwana ni nguvu yako.  Nataka kuhakikisha kwamba uko tayari kupambana! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.