... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kusubirisha Hukumu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 6:37 Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.

Listen to the radio broadcast of

Kusubirisha Hukumu


Download audio file

Unajua, inashangaza mno namna tunavyopenda kuhukumu watu wengine.  Sura zao, maumbile yao, maneno na hata matendo yao.  Kusema ukweli, kila siku tunahukumu watu mara nyingi tu.

Ebu, fikiria.  Unakutana na mtu kwa mara ya kwanza.  Huwa unamsomaje kwa haraka haraka?, kusema ukweli kuna watu wanavutia bila kujali utofauti wa maumbile yao au muonekano wa sura.

Lakini hata kwa watu tunaojuana nao kwa muda mrefu, wanaposema kitu ambacho hatukubaliani nacho huwa tunawahukumu.  Mara moja tunamchapa kwa mitazamo yetu na mapokeo yetu kwa kuhukumu kikatili maoni yake na mtazamo wake.  Migogoro inaanzia hapo hapo.  Sasa, kama tungekumbana na hali hiyo kwa njia tofauti, ingekuaje? 

Luka 6:37  Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. 

Ingekuaje kama tungeahirisha hukumu na kusubirisha maamuzi?  Ingekuaje kama tungesamehe badala ya kuhukumu?  Ingekuaje kama wakati kama huo, tunaruhusu ubinadamu wa mwingine kutudai huruma inayostahili kwa kuwa na yeye anamatumaini na ndoto, pamoja na mapungufu na madhaifu kama vile tulivyo sisi. Je! Mahusiano yetu na wengine si yangekuwa tofauti kabisa?  Ulimwengu wetu si ungebadilika kweli?

Mgogoro unaanzia pale tunapohukumu wengine.  Huruma huwa inaanzia pale tunapoahirisha hukumu.  Mgogoro unaanzia pale tunapojitenga na ubinadamu wa wengine na kuwatendea vibaya.  Upendo unaanzia pale tunapokuwa na shauku ya kutaka kuelewa kwanini wanatamka au kufanya vile.  

Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.