... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuthubutu Kuwa Tofauti na Wengine

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Timotheo 3:12,13 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. Lakini watu wabaya na wadangayaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.

Listen to the radio broadcast of

Kuthubutu Kuwa Tofauti na Wengine


Download audio file

Yesu aliwaahidi wanafunzi wake mambo mengi, kuna ahadi moja ambayo sijui kama unaweza kuipokea kwa shangwe na vigelegele huku ukisema haleluya.  Ahadi hiyo ni hii, kama walimwudhi yeye (na kweli aliudhiwa) basi na sisi watatuudhi.

Labda si dhana yakukufurahisha, sidhani.  Lakini ni kweli, Mahali panapofanana na sehemu ninayoishi, Wakristo wamekuwa na amani miaka ya kutosha.  Mahali pengine, wameudhiwa vibaya.  Haijalishi unaishi wapi au uko katika mazingira gani, tayari mateso yapo au yanakuja hivi karibuni. 

Hata kama kwa sisi tunaoishi kwenye utilivu, swala hili la mateso na kuudhiwa kuongezeka, lisingetushangaza kwa sababu si jambo jipya.  Kama vile mzee mwenye busara, Mtume Paulo alivyomwandikia Timotheo mwanae:

2 Timotheo 3:12,13  Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.  Lakini watu wabaya na wadangayaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. 

Ni akina nani watakaoudhiwa?  Ni wote wapendao kuishi maisha ya utaua katika Kristo Yesu. 

Kwahiyo inaonekana kwamba mtu akitaka kujiepusha na mateso, aache kujaribu kuishi maisha ya utaua katika Kristo; yaani, ajaribu kuwa sawa na wa-ulimwengu, asionekana kuwa tofauti.  Si ninaweza kuamini Yesu ki-sirisiri na kuonekana kama watu wengine hadharani?  Ni mbinu wa kukwepa mateso. 

Lakini kama vile Charles Spurgeon alivyosema:  Itakuwa siku ya huzuni mno kwa ajili ya kanisa na hata kwa ajili ya ulimwengu, hakutakuwa na utofauti kati ya mtoto wa Mungu na mtoto wa ulimwengu huu. 

Wewe ni nuru ya ulimwengu.  Acha kujaribu kufanana na watu wa ulimwengu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.