... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Leta Tabia Yako Mbele za Bwana

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 5:16 Lakini Yesu alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.

Listen to the radio broadcast of

Leta Tabia Yako Mbele za Bwana


Download audio file

Kuna ukweli wenye nguvu ambao haipaswi utuponyoke.  Mungu anataka kutusaidia, wewe na mimi, ili tuweze kuishi kwenye ushindi ule Yesu alioupata kupitia kifo chake na ufufuo wake ambao anataka kutupa na sisi.  Ushindi dhidi ya dhambi zetu na ushindi juu ya mazingira yetu.

Kuna kweli zingine haitupasi kuzisahau, ni kwamba sisi tukikubali kushawishika na dhambi kupitia tabia mbaya au mazoea mabaya, lazima itatuibia ule ushindi kila siku. 

Ndio maana tunapaswa kabisa kuleta maisha yetu, tabia zetu, matamanio yetu, shauku zetu na mipango yetu mbele za Mungu. – na kama umeshanisikia nikiyasema, basi utaendelea kuyasikia tena mara nyingi tu – kuna aina moja tu ya maombi Biblia inayotufundisha, ni maombi yaletayo matokeo yenye nguvu. 

Luka 5:16  Lakini Yesu alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba. 

Sasa Yesu mwenyewe hakuwa na dhambi hata kidogo lakini mara nyingi ilibidi aende wapi?  Mahali pasipokuwa na watu.  Kwanini?, ili aweze kuomba faraghani.  Kwa kuwa aliweka kando uweza na utukufu wake pale  alipofanyika mtu, alifahamu kwamba katika maombi ya faragha, ndipo anapoweza kupata hekima na uweza aliohitaji kutimiza katika yote aliyoitiwa. 

Si zaidi sana basi, wewe na mimi tunavyohitaji kuleta mambo yetu yote mbele za Mungu katika maombi?  Hususani  zile tabia sugu ambazo  kila mara huwa zinatupelekea kutenda dhambi. 

Uzilete mbele za Mungu katika maombi.  Pokea uwezo wake pamoja na hekima yake ili viweze kuvunja nguvu za tabia na kukuweka huru.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.