... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mamalaka ya Mauti Imekufa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Warumi 6:7-9 Kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha fufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.

Listen to the radio broadcast of

Mamalaka ya Mauti Imekufa


Download audio file

Hivi, umewahi kujiuliza maisha yako yangekuaje leo kama Yesu asinealikutana na wewe njiani?  Kama usingesikia sauti yake ikikuita ili akupe uhuru wake, amani na kuishi naye milele?

Ni maswali nimeyojiuliza mara nyingi kwasababu siku Kristo aliyoonekana kwangu ilikuwa punde tu nijiue kwa kujitupa chini kutoka ghorofa ya nane ya hoteli. 

Kama Yesu asingegusa moyo wangu muda ule ule… nadhani nisingekuwepo leo. Nadhani ningekuwa Jehanamu tayari mahali ambapo ningekaa huko milele na milele. 

Nilitaka kufanya hivyo kwasababu nilikuwa nimezama kwenye matope ya dhambi na hadi pale mtu aliyeupokea msamaha wa Mungu alipoonekana kwangu. Bila dhabihu ya Kristo pale Msalabani, sadaka inayotupatanisha na Mungu; hawezi kushinda dhambi na kuepuka na matokeo yake ambayo ni mauti ya milele. 

Warumi 6:7-9   Kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.  Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye; tukijua ya kuwa Kristo akiisha fufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena. 

Kifo kilishindwa kumshikilia na kumkandamiza.  Na kama umemwamini Yesu, nisikilize tafadhali ni muhimu sana; wewe pia utaishi milele mbele za Uso wa Mungu.  Hii ndiyo hatima yako … kama umeweka tegemeo lako kwa Yesu. 

Rafiki yangu, ninakusihi, popote pale umepofikia maishani mwako, jitupe kwenye neema na rehema za Mungu ndani ya Yesu Kristo.  Kwasababu ndani yake, mauti haina mamlaka juu yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.