... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mbeleni Kuna Siku za Furaha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

2 Wakorintho 4:16,17 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.

Kumbe!, Imeshakuwa Jumapili na ninatumaini kwamba tumetenga muda wa kumwabudu Mungu na kupumzika pia, jambo linalohitajika kwa mwanadamu.  Halafu Jumapili hii, ninawiwa kukushirikisha neno lenye nguvu la kukutia moyo.

Maisha haya, huwa yanatugharimu. Kuna maumivu, mikwaruzo, kuchubuliwa ni hali tunayoipata kuanzia kuzaliwa kwetu hadi kufa. 

Mtume Paulo alikuwa ametoka kuelezea rafiki zake habari za mateso makubwa yaliyompata kabla ya kuandika mistari ifuatayo: 

2 Wakorintho 4:16,17  Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.  Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana. 

Kwa Kawaida ninapenda kufanya mazoezi lakini siku baada ya siku najitambua kwamba utu wangu wa nje unachakaa. Wewe pia mwili wako utachoka, utazeheka. Lakini Neno la Mungu linakwambia leo usikate tamaa kwasababu kadiri unavyozidi kumtegemea Yesu, ndipo utu wako wa ndani – na ndio sehemu muhimu – unafanywa upya siku kwa siku. 

Na hayo yote ni kwa ajili ya kukuandalia utukufu wa milele uzidio usioweza kulinganishwa na chochote … na utaendelea milele na milele daima. 

Kwahiyo, rafiki yangu, usikatishwe tamaa. Mungu yuko pamoja nawe na anakubadilisha … kwa sababu mbeleni kuna siku za furaha.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.