... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mungu Ndiye Ajuaye Peke Yake

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 139:23,24 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, unijaribu, uyajue mawazo yangu; uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, ukaniongoze katika njia ya milele.

Listen to the radio broadcast of

Mungu Ndiye Ajuaye Peke Yake


Download audio file

Mara nyingi wewe na mimi tunadai kwamba tunajijua vizuri, tunajielewa vya kutosha uwezo tulio nao pamoja na mapungufu yetu, ahahaha

Lakini hata kama tunajidai hivyo, inabidi tuseme ukweli, lazima tukiri kwamba hatujijui vizuri tena vya kutosha. Mara ghafla “Waah!”  Kitu kinakugonga bila kutazamia, unakipokea vibaya, unamkasirikia mtu, unaharibu mahusiano na fulani, unamhuzunisha Mungu.  Halafu makusudi yako yote mazuri yanaanguka chini. 

Kwanini sikutazamia tukio lile?  Kwa nini nilifanya hivyo?  Nilikuwa ninawaza nini? 

Hayo yalimtokea Mfalme Daudi,

Zaburi 139:23,24  Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, unijaribu, uyajue mawazo yangu; uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, ukaniongoze katika njia ya milele. 

Sisi ni viumbe wenye tabia nyingi, mchanganyiko wa matukio mbalimbali (mema na mabaya) katika yaliyotupa maishani na kutufanya tulivyo leo, watu wenye matumaini na maumivu, furaha na matatizo.  Hayo yote yanavuruga mioyo yetu hata fikra zetu na kuathiri roho zetu. 

Ukweli ni kwamba hatujijui wala kujitambua vizuri kama Mungu anavyotufahamu.   Ndio maana ni busara kumuomba Mungu kutuchunguza, ajue mioyo yetu, atujaribu, ili ahakikishe kwamba tunaelekea njia sahihi.  Kwasababu yeye ndiye anayetufahamu kweli kweli.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.