Namna Mtu Anavyokuwa Mfano Mbaya
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 4:19,20 Sisi twapenda kwa maaana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
Sipendi kuonekana mnafiki. Si kwasababu mimi ni mwepesi wa kuumia au najali vile watu wanvyonisifu!, hapana, ni kwasababu nikiwa mnafiki, siwezi kusababisha Injili ya Yesu Kristo ipate heshima zake.
Sasa, kwa kuwa Injili kuna wakati inaleta utengano na kwa kuwa Biblia inafundisha wazi kuhusu dhambi na toba, ni kikwazo kwa wenye dhambi wengi. Watakutukana. Huwezi kukwepa hayo.
Lakini unapooona picha ya mtu Facebook, huku akisimama karibu na gari lake nyekundu lenye matangazo kama, “Tubuni!” au “Upendo wa kweli”, au “Yesu anarudi hivi karibuni”, au “mrudie Mungu” … halafu baadaye aweke picha ya rais wake huku akimtukana vibaya … basi, mtu huyo ndiye mnafiki, bila shaka.
Tabia kama hiyo, si kwamba inazalilisha Injili tu, lakini pia nadhani Mungu hawezi kupendezwa nayo.
1 Yohana 4:19,20 Sisi twapenda kwa maaana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
Kama ulikulia nyumbani ukiwa na kaka zako na dada zako, utajua kwamba mara nyingi hamkuweza kukubaliana, kuna wakati mnapigana, mlipigana na kugombana.
Mungu anaelewa hali hiyo pale alipomsukuma Yohana kuandika maneno hayo, si kwa ushauri tu, bali kama agizo.
Kama kweli tunampenda Mungu, lazima tupendane sisi kwa sisi kama ndugu.
Usiwe mnafiki!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.