... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Neema Inabadilishaje Mtazamo Wako?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 1:3-8 Atukuzwe Mungu, Baba wa 
Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi.

Utaniruhusu nikikuulize swali?  Kwa kipimo cha sufuri hadi kumi, ni kiasi gani neema ya Mungu iliyoko ndani ya Yesu Kristo imekubadilisha kabisa?  Sitanii.

Sasa, kama kweli unamwamini Yesu na kutamani maisha bora – hata ukijua kwamba kumfuata Yesu kutakugharimu kama vile yeye mwenyewe alivyosema – lakini ikiwa neema ya Mungu bado haijabadilisha maisha yako basi utakuwa una matatizo kweli kweli.  

Waefeso 1:3-8  Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.  Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.  Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.  Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.  Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi. 

Neno hilo, Neno la Mungu ndilo jambo la muhimu ningeweza kukushirikisha leo.  Maneno yangu ni hafifu. liachie Neno la Mungu liingie kwenye kiini cha moyo wako.  Ruhusu baraka, fadhili na neema ya ajabu ya Mungu vijae ndani ya moyo wako, vivunje minyororo, vikuweke huru uwe yale yote aliyokusudia uwe wakati alipokuumba.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.