... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Neema Inayozidi Tuwazayo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 1:3-6 Atukuzwe Mungu, Baba wa 
Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.

Listen to the radio broadcast of

Neema Inayozidi Tuwazayo


Download audio file

Kadiri mtu anavyozidi kuchunguza na kutafakari neema ya Mungu, ndivyo inavyozidi kubadilika. Nadhani ndio lengo la Mungu.  Neema yake lazima ibadilishe maisha yetu kabisa!

Na sisi tumechukua siku kumi tukichunguza kwa pamoja habari ya neema ya Mungu, tukaikumbatia, tukijua namna imevyotubadilisha tangu tulipoamini yale yote Yesu aliyotutendea. 

Waefeso 1:3-6  Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.  Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.  Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. 

Ndiyo. tumeshabarikiwa na baraza zote za kiroho ndani ya Yesu.  Ndio, tulichaguliwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa ili dhambi zetu zifutwe, tuishi maisha ya utakatifu bila hatia katika safari yetu kwenda kukaa mbele za Mungu milele.  Lakini chunguza pia mwisho wa mistari hiyo … 

Alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.  Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.  

Wewe na mimi, tumekusudiwa kufanywa watoto wa Mungu kupitia neema yake tukufu aliyotukirimia.  Neema juu ya neema. 

Kawaida, tungepaswa kuwa wafu katika dhambi zetu, wewe na mimi.  Lakini sasa tu hai ndani ya Kristo. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.