... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Neema ya Mungu Iliyo Kali

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 13:14-17 Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akajibu akasema, Enye wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye.

Listen to the radio broadcast of

Neema ya Mungu Iliyo Kali

Download audio file

Basi, tumeanza wiki hii isiyoeleweka iliyo kati ya Krismasi na Mwaka Mpya.  Sehemu ambayo hakuna mengi yanayoweza kutendeka tukitafakari mwaka uliopita na kutazamia mwaka mpya unaokuja.

Kama uliweza kufuatana nami wiki iliyopita, basi utafahamu kwamba tumekuwa na mafundisho kuhusu neema, kweli, neema ya Mungu ni kubwa mno.  Huwa inabadilisha maisha ya mtu. Turudie mada hiyo kwa sababu neema hii ya Mungu imekusudia kufuta dhambi zako zote, na kufungua mlango ili uweze kuingia maisha mapya huko mbele yako. 

Luka 13:14-17  Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato.  Lakini Bwana akajibu akasema, Enye wanafiki, kila mmoja wenu, je!  Hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha?  Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?  Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye. 

Yesu alimponya yule mwanamke hata kama hakuendana na kanuni za dini.  Hii ni neema kali, neema ile ile ya kuponya amekuandalia wewe. 

Neema inayopindua mambo.  Neema iliyo tayari kwa ajili yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.