... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

ni Afadhali Kuteswa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 3:17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.

Listen to the radio broadcast of

ni Afadhali Kuteswa


Download audio file

Kuteswa ni mada ambayo ninapenda kuirudia mara kwa mara, nataka nielemishwe zaidi na kupiga hatua mbeleni na ninatarajia kwamba inaweza kukusaidia pia katika hatua hizo.  Ni kwa sababu tunapopata mateso, ndipo tunapoweza kupata fursa kubwa kuliko zote Mungu anazotukirimia.

Mwanariadha yoyotee atakwambia kwamba anateswa sana wakati wa mazoezi.  Ili mtu ajenge misuri, ni lazima aumie.  Kujifunza kustahimili inaumiza.  Lakini kwa wanariadha ni mateso yenye malengo maalum.  Ni mateso kwa ajili ya kuboresha ujuzi na ustadi wao katika michezo ili waweze kuwa wepesi zaidi.  Ndio maana wanakubali kujitesa. 

Na hivyo ndivyo ilivyo katika maisha yetu pia.  Tunajua kwamba vipindi vigumu ndivyo Mungu huwa anavitumia kufinyanga tabia zetu vizuri; akitufundisha kumtegemea zaidi.  Ni kipindi kizuri cha kutulainisha na kututengeneza ili tuweze kufanana zaidi na Yesu. 

Lakini – kwa nini kuna “walakini siku zote? – mara nyingi mateso yanatokana na uonevu na kule kuonewa kunasabasha kiburi chetu kipande.  Yaani, kunyimwa haki kunatupa mtazamo mbaya  unaoweza kuzuia mafao yale Mungu aliyotaka kuingiza katika tabia yetu kupitia mateso yale.  Daima, kiburi kinazuia baraka za Mungu, si kweli? 

Kwa hiyo, hii ikitokea maishani mwako, basi sikiliza vizuri: 

1 Petro 3:17  Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. 

Petro aliandikia maneno haya kwa Wakristo waliokuwa wanateswa vibaya na kunyimwa haki zao kwasababu ya imani zao ndani ya Yesu.  Kama Mungu anaruhusu kipindi cha mateso kikujie, na kama ni mapenzi yake, basi yapokee kwa furaha. Uteswe na moyo mweupe na kwa mtazamo mwema hata kama inaonekana kwamba umeonewa sana … kwa sababu Mungu anakuandalia kitu kizuri sana. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.