... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Akina nani Wataketi Kwenye Kiti cha Enzi?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ufunuo 3:21,22 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Listen to the radio broadcast of

Ni Akina nani Wataketi Kwenye Kiti cha Enzi?


Download audio file

Ni kama umilele uko mbali sana, sindiyo?  Kwanini?  Labda ni kwa sababu tumezama sana kwenye maisha ya kila siku, ko swala la “uzima wa milele” ni vigumu kwetu kulitafakari.

Lakini, ukweli ni kwamba, maisha yako ya kila siku bila kujali unafanya nini yanahusu kabisa namna utakavyoishi milele kwasababu kuna vita inaendelea ili kuamua ni yupi atamiliki nafsi yako. 

Kwanza, Shetani daima anajaribu kukuvuta utoke kwa Yesu.  Yeye anatamani ushi naye milele.  Pia kuna tamaa zetu wenyewe ambazo tukiziruhusu tu, basi zingetupelekea kutenda dhambi hadharani na hatimaye kufuata njia ile ile ya uharibifu bila Shetani kuhangaika.

Tena isitoshe, dunia inatupigia kelele – tena kwa sauti kubwa – tuache kumtegemea Yesu aliyepitwa na wakati.  Kwahiyo, tuna adui wengi wa kupambana nao katika safari yetu.  Lakini tuzo … tuzo itatutosheleza kabisa tusipozimia katika mashindano hayo. 

Ufunuo 3:21,22  Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.  Yeye aliye na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. 

Ni akina nani wataketi na Yesu milele kwenye kiti chake cha enzi?  Ni yule ashindaye.  Ni yule anayejitahidi kwenye mapambano ya maisha.  Ni yule anayeshinda vikwazo vyote vilivyowekwa mbele yake na ulimwengu huu na adui.  Ni yule anayestahimili hadi mwisho … kama alivyofanya Yesu. 

Usisalimu amri. tuzo itakutosheleza. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.