... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kila Tatizo Lina Lengo Lake

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ayubu 23:10,11 Lakini yeye aijua njia niendayo; akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

Listen to the radio broadcast of

Kila Tatizo Lina Lengo Lake


Download audio file

Wakati tunapitia kipindi cha matatizo mara kwa mara, dhana au swali linalokuja ni hili:  Kwa nini hayo yamenipata mimi?  Ni swali ambalo linahitaji kujibiwa.

Haujambo? Mimi ni Berni Dymet ninakukaribisha kwenye kipindi hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA.    

Binadamu hawezi kuepukana na mateso ya ulimwenguni, Hakuna mwanadamu hata moja aishiye duniani ambaye hajateswa.  Kuanzia maumivu ya kuzaliwa na maumivu yote ya utoto na ujana wake … hadi anakuwa mtu mzima, bado anapata shida na mateso.

Nisingeshangaa kusikia kwamba, wakati ninakuchorea picha hii ya mateso, ungekuwa unakumbuka kipindi Fulani cha Maumivu katika maisha yako.

Mungu wangu, kwa nini?  Kwa nini mimi?  Kwa nini sasa?

Kama umewahi kusoma kitabu cha Ayubu katika Agano la Kale, utafahamu kwamba kinalenga mateso yake.  Ayubu alikuwa mwadilifu.  Alimheshimu Mungu. Lakini Mungu aliruhusu ateswe vibaya sana.  Kupitia sura moja hadi nyingine, Ayubu anauliza rafiki zake, na kumuuliza Mungu pia … Ni kwa nini?  Lakini alifikia mahali pa kujibu swali lake:

Ayubu 23:10,11  Lakini yeye aijua njia niendayo; akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.  Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

Kumbe.  Ilionekana Mungu alimjua vema Ayubu, kama Ayubu aliishi kama Mungu alivyotaka, hata kama hakuwahi kuacha kumfuata Mungu … bado Bwana alimjaribu.

Wakati tunapitia vipindi vigumu, ni Mungu anayepima imani yetu kwake.  Anapima uhalali wa nia yetu kumheshimu kuliko yote, licha ya tatizo lote lile. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.