... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ukitenda Mema

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Petro 2:15 Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu.

Listen to the radio broadcast of

Ukitenda Mema


Download audio file

Tunaishi kwenye ulimwengu ambao yale tuliyokuwa tunajua kwamba ni maovu –  kama uroho, tamaa, uzinzi na kadhalika – sasa yanaitwa mazuri tena yanapongezwa.  Ole kwa atakayejaribu kusimama kinyume cha mtazamo huo.

Ni hali ambayo kusema wazi, ninaelewa vizuri sana kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa mmoja wao.  Kwa sababu kabla sijabadilika kuwa Mkristo, nilikubali kwamba yale Mungu anayoyasema kuwa mema ni mema kabisa, na yale anayosema kuwa maovu ni maovu kabisa, nilikwazika mno na wale Wakristo waliojifanya kuwa bora kuliko watu wengine. 

Wakati ule, hata kama singaliweza kueleza kwa kutumia maneno haya, uadilifu wao ulichoma dhamiri yangu kwasababu ndani kabisa nilijua kwamba dhambi zangu zilikuwa mbaya mno, maovu yangu yalikuwa maovu kweli, lakini sikutaka kuziacha.  Kwahiyo niliwaudhi Wakristo niliofahamiana nao.  Hii ilikuwa matokeo. 

Mtu akisimama kinyume cha uonevu, mtu akikataa kucheka kwa utani mchafu, mtu akikataa kusema uongo, au mtu akikataa kukubali uasherati unaoletwa siku hizi kama biashara … basi ulimwengu utamkataa kabisa.  Kwa hiyo, jibu linapatikana wapi? 

Je! Tuache kutenda mema?  Sidhani. 

1 Petro 2:15  Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu. 

Hatimaye wema utadhihirika.  Wema wako dhidi ya uovu na gharama utakaolipa kwa msimamo wako, vitatikisa wengi kuliko unavyofikiria.  Wema wa wale Wakristo niliokuwa ninawatesa zamani, unyenyekevu wao, jinsi walivyonipokea na kunisamehe … vyote viliunganika pamoja kwa kunivuta nimwamini Yesu. 

Kwa vyo vyote tenda mema.  Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.