... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usirupuke Kutenda Maovu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 14:17 Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.

Listen to the radio broadcast of

Usirupuke Kutenda Maovu


Download audio file

Kuna wakati tunatenda kwa ujinga bila hata kufikiria, mambo yanaweza kuwa shwari kama kawaida halafu ghafla, kitu kinatuchokoza na mara moja tunarupuka kutenda mabaya.

Ni ajabu mno namna ambavyo siku njema inaweza kubadilika na kuwa msiba mkubwa kwasababu tu kitu fulani kimechochea.  Tunakwazika na jambo fulani, tukio linatokea, linatutia jazba, jambo ambalo hakuna aliyetazamia. 

Mithali 14:17  Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; na mtu mwenye hila mbaya huzirwa. 

Hapo Mfalme Sulemani anaeleza habari ya maovu ya aina mbili.  Uovu unaoripuka na uovu wa hila unaofichwa ndani ya mtu anayejiandaa kulipiza kisasi. Huu wa pili tutauongelea kesho, lakini kwa sasa tuongelee uovu wa kwanza. 

Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga. 

Nikisema ukweli, asili yangu mimi ni mtu anayekasirika haraka.  Mimi ni mchangamfu ninayefanya mambo yote haraka.  Ninafikiri kwa haraka.  Hata ninapotembea kwa mihguu huwa natembea haraka-haraka.  Yaani Muitikio wangu ni wa haraka, ndivyo nilivyo.  Labda wewe uko tofauti.  Pengine wewe ni mtaratibu, unafanya mambo baada ya kutafakari kwanza. Lakini hata hivyo, nina amini kuna mambo mengine ambayo yanaweza kukuchukiza mno na ukatenda kwa haraka. 

Ni yapi yanaweza kukuchukiza na kusababisha uripuke vibaya?  Je!  Mwitikio kama huo utakusaidia kweli?, Utakuletea sifa njema na kuboresha mahusiano yako? 

Kuona hasira upesi kunasabisha mtu kutenda kwa ujinga. 

Jaribu kutambua ni yapi yanayokuchukiza.  Panga mwitikio wa tofauti na kawaida yako.  Acha kutenda kwa ujinga. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.