... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usishikwe na Hofu, Wala Usihangaike

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 46:1-3 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.

Listen to the radio broadcast of

Usishikwe na Hofu, Wala Usihangaike


Download audio file

Tukitumia mfano wa mpira wa mguu, mtu anapopigwa na mpira wa tumbo anaweza kukosa pumzi, sikiliza kuna wakati maisha yanakuwa hivyo. 

Mimi nimeshawahi kupigwa na mpira wa tumbo mara tatu nilipokuwa golikipa zamani, kusema ukweli haipendezi hata kidogo, hadi leo bado ninakumbuka jinsi nilivyokuwa na hofu pale nilipokuwa siwezi kupumua.

Kinachosababisha hali hiyo iwe mbaya zaidi ni kushitushwa.  Yaani mtu hategemei kabisa – ghafla anapigwa sehemu ya mishipa ya fahamu. 

Angalia, Kuna mambo kwenye maisha huwa yanatokea ghafla ambayo yangesababisha tushikwe na hofu kuu.  Yamewahi kututokea na bila shaka yatatokea tena.  Sasa mtu anaposhikwa na mahangaiko kama hayo, ni kama imani yake inatoweka pia, sijui kama umeshaona?  Mahali ambapo mtu angehitaji imani yake itende kazi, ghafla inatoweka! 

Hivi karibuni nilitikiswa niliposoma yale yaliyoandikwa na Martin Lloyd Jones akisema:  Imani ni kukataa kuhangaika.  Kumbe, kusema hivi kunaenda sambamba na Maandiko: 

Zaburi 46:1-3  Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.  Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.  Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. 

Sidhani kama kuna tukio linalotisha kama tetemeko la ardhi – yaani nchi inatikiswa hovyo, milima inabomoka na kuanguka ndani ya bahari, maji yanavuma na kuumuka.  Jamani!, Lakini mtunga Zaburi anastahimili, akiwa shupavu anakataa kushikwa na hofu kuu. Kwasababu gani? kwasababu … Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.  

Uwe kama mshupavu.  Usiogope.  Umwamini Mungu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.