... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiwe Kama Chakula Kilichochacha

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 63:1,3 Ee Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji … Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; midomo yangu itakusifu.

Listen to the radio broadcast of

Usiwe Kama Chakula Kilichochacha


Download audio file

Kila uhusiano tulio nao maishani mwetu, unaweza kufika mahala pa kupoa.  Pale palipokuwa na mahusiano mazima yenye hisia kali, mahusiano yaliyokuwa na faida – ikiwa ya mwenzi au rafiki … au hata na Mungu – kuna siku yanakuwa hayana umuhimu tena kama yalivyokuwa.

Najiuliza kama unaweza kufikiri juu ya mahusiano maishani mwako ambayo kwasasa yameshapoa sana.  Halafu unakaa pale ukijiuliza … Je! imekuwaje? 

Na ukweli ni kwamba kwa watu wengi waliofanya maamuzi moyoni kwamba wataishi kwa ajili ya Yesu nao mahusiano yao na yeye yamepungua hadi kupoa. Kama chakula kilichochacha. Ki vipi yaliweza kufika hapo? 

Kwanza, tujue kwamba shughuli za kila siku na hali ya kupambana na changamoto za maisha vinaweza kusababisha mtu aelekee huko. Yamkini unajikuta leo jangwani huku ukijiuliza utatokaje hapo. 

Mfalme Daudi alikuwa anapitia sehemu kama hiyo. Na kweli alikuwa anajificha nyikani,  Kwahiyo aliomba dua hii kwa Mungu: 

Zaburi 63:1,3  Ee Mungu wangu, nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu wakuonea shauku katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji … Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; midomo yangu itakusifu. 

Mimi ninaona kuna sababu moja kubwa isababishayo mahusiano yetu na Mungu kupoa ni kwasababu hatuna tena shauku moyoni ya kumtafuta.  Macho yetu yanalenga mazingira ya kukatisha tamaa yanayotuzunguka jangwani pale tulipo, halafu tunasahau kwamba pale pale, fadhili za Mungu ni njema kuliko uhai. 

Usipoe.  Umwonee kiu Yesu! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly