... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Wakati Mungu Haonekani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ayubu 23:8-11 Tazama, naenda mbele, wala hayuko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; hujificha upande wa kuume, hata nisimwone. Lakini yeye aijua njia niendeayo; akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

Listen to the radio broadcast of

Wakati Mungu Haonekani


Download audio file

Sote tumeshapitia vipindi ambavyo Mungu alionekana kama haonekani kwenye maisha yetu.  Kinadharia, mtu anaweza kuamini kwamba Mungu hawezi kumpungukia wala kumwacha kabisa.  Lakini ki-utendaji, yuko wapi sasa?  Kwanini ninaweza kujisikia mpweke?

Labda hautanielewa nikikwambia kwamba hata mimi ambaye ni mwalimu wa Biblia ninaweza kupatwa na hali hiyo.  Berni, si unatembea karibu na Mungu kila siku?, ahahaha 

Acha nisema wazi kabisa.  Hali ya kuona kwamba “Mungu haonekani” huwa inanitokea na mimi.  Ni jambo linaloweza kumpata mtu yeyote.  Bila shaka Mungu bado yuko nasi mahali, hiyo ndio ahadi yake. 

Lakini, pamoja na hayo, bado Mungu anaweza kujisogeza nyuma asionekane kwenye fikra zetu, huwa anafanya hivyo mara kwa mara, hatimaye sisi tunabaki na.  Katika Agano la Kale, Ayubu alipata mateso makubwa.  Alimezwa na maumivu makali na misiba mikubwa.  Kwenye Kipindi kama hicho kusema ukweli ni rahisi mtu kujiona mpweke. Hivi ndivyo alivyojieleza Ayubu wakati ule: 

Ayubu 23:8-11  Tazama, naenda mbele, wala hayuko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona; hujificha upande wa kuume, hata nisimwone.  Lakini yeye aijua njia niendeayo; akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.  Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. 

Je!,  Ni kwanini Mungu anajisogea nyuma mara kwa mara.?  Ni lengo la kutupima, kuhakikisha kwamba sisi ni dhahabu safi.  Kamwe usiache kumfuata.  Hata kama humuoni, bado yuko pamoja nawe. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.