Kitu Mungu Anachokitaka
Add to FavouritesAmosi 5:21-24 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vianda vyenu. Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.
Kama vile cho chote kile kinaweza kubadilishwa kuwa njia ya kuchuma fedha, Ukristo pia unaweza kuwa kama biashara. Yaani mali ya makanisa baadhi yanashangaza mno. Kwa hiyo ni rahisi wachaMungu kama wewe na mimi kushawishika na mfumo ule.
Labda unafikiri kwamba nimekuwa mkali, sindiyo? Lakini kanisa la Ukristo duniani limekalia matriliyoni ya dola ukizingatia viwanja vyao na rasilimali zingine, sehemu yake yasitumiwa vizuri hata kidogo. Nikisema ukweli, simu yangu imejaa matangazo ya kongamano hii, upigaji muziki ule, mkutano maalum pale, unabii fulani … na kadhalika.
Ni kweli, kanisa linahitaji rasilimali ili litende kazi ya Mungu. Ni kweli, kuwa ni mikutano mbali mbali duniani kujifunza Neno la Mungu na kumwabudu ni muhimu. Lakini ni rahisi mtu kupelekwa na utendaji kazi wa biashara ya Ukristo inayosababisha watu wajiinue na kupoteza dira wasipambanue tena mapenzi ya Mungu hasa.
Sasa, Mungu anataka nini? Yafuatayo yanaeleza anachokitaka yeye:
Amosi 5:21-24 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini. Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vianda vyenu. Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu.
Haina makona mengi. Umwabudu Mungu kutoka moyo wako wote. Ishia imani yako katika upendo kwa kutenda haki na kuwa mwadilifu. Usivutwe tena na shamrashamra.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.