Kufuta Kabisa Umbeya
Add to FavouritesMithali 11:13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.
Umbeya una uwezo kumharibia mtu sifa. Udaku kidogo hapa, mnong’ono pale na baada ya muda mfupi tu, kiwanda kile cha umbeya kinaanza kutoa uvumi wake kwa wingi. Ni nini kinachotusukuma kukubaliana na mambo hayo?
Ukweli ni kwamba sisi sote tunayo mambo mengine ya aibu maishani mwetu ambayo tusingependa yaingizwe kwenye mzunguko wa kiwanda cha umbeya.
Ebu fikiria ingekuaje kama Mungu angepiga domo na kudakua mambo yako? Anajua kila kitu kinachokuhusu, kila jambo ulilowahi kufikiria au kusema au kutenda. Ingekuaje kama angefunua siri zako zote kwa yo yote yule na kwa watu wote?
Afadhali sivyo alivyo. Afadhali hawezi kufanya hivyo. Kwa kuwa anatuhurumia kila mmoja wetu, Neno lake, yaani Biblia inakataza kabisa umbeya, tena inaukataza mara nyingi tu.
Mithali 11:13 Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; bali mwenye roho ya uaminifu hisitiri mambo.
Je! Ungemwamini mtu ambaye unajua kwamba ni mdaku? Huwezi kumwamini, si kweli? Na wewe unatakiwa ujulikane kuwa mtu mwaminifu kama hata mimi ninavyotaka niwe. Kuna njia ya kujenga sifa ya kuwa mwaminifu. Ni kustopisha mara moja maneno ya msengenyo yasiendelee.
Kama vile mtu fulani alivyosema, umbeya unakufa wakati unafika kwenye masikio ya mtu mwenye hekima. Kwa hiyo, kazini, katika rafiki zako hata ndani ya familia yako, unawezaje leo hii kuweka breki udaku usiendelee tena?
Uwe mtu yule mwenye busara. Uwe mtu yule anayekataa maneno ya umbeya yasienee. Uwe mtu yule anayeonyesha upendo wa Mungu kwa kufunga midomo yako.
Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; bali mwenye roho ya uaminifu hisitiri mambo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.