... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Acha Fitina

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:10-13 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Listen to the radio broadcast of

Acha Fitina

Download audio file

Haijalishi ni watu akina gani wakikusanyika pamoja, wala hailishi kundi lao lina lengo gani, lazima mafarakano yatajitokeza. Ugomvi utafuata na hatimaye watagawanyika makundi-makundi.

Hua inatokea katika familia, kazini na katika mashirika ya umma.  Na hatuwezi kusita kusema kwamba inatokea ndani ya makanisa pia … hata kama shauku la Mungu ni kwamba watu wake wawe na umoja.  Ndiyo maana zamani alimwambia Mtume Paulo aandike maneno yafuatayo:

1 Wakorintho 1:10-13  Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.  Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.  Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.  Je!  Kristo amegawanyika?  Je!  Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu?  Au je!  Mlibatizwa kwa jina la Paulo?

Sasa je!  Sisi, kama watu wateule wa Mungu, tumefaulu kiasi gani kutimiza lengo lake kwetu kuwa na ushirikiano, kuwa na umoja?  Ebu sikiliza matokeo ya utafiti uliofanyika na Senta ya Kutafiti Ukristo Duniani.  Wamejaribu kuhesabu dhehebu za Kikristo zilizopo ulimwenguni na wamepata idadi ya 45,000.  Si ajabu kuwa na dhehebu nyingi hivyo?!

Nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.    

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.