Ahadi ya Amani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Mambo ya Nyakati 22:9 Tazama, utazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe; nami nitamstarehesha mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake.
Dunia hii inaweza kuahidi vitu vingi sana – ajira nzuri, mafanikio, pesa, likizo, gari mpya, hata viatu vipya au vipodozi vizuri. Lakini mwisho wa siku, hakuna vinavyoweza kukupa … amani.
Kila mtu anatamani kuwa na amani maishani mwake. Ni nani anayetamani migogoro? Ni yupi angetamani kuishi na wasiwasi? Ni yupi angetamani kuwa na mashaka kila wakati anadaiwa kodi ya nyumba au akifikiri jinsi atakavyopambana na changamoto za kesho? Kwa kweli kuwa na amani ni thamani kubwa mno.
Na hata kama utajiri unaonekana kuwa na uwezo wa kuleta amani, ni ahadi bandia mtu akishuhudia orodha ya matajiri wanaojinyonga – wachezaji maarufu wa filmamu, waimbaji mashuhuri, hata watu wa familia za kifalme.
Kwa kweli kuwa na amani ni kitu muhimu chenye thamani kubwa, Mungu aliahidi watu wake mara nyingi katika Neno lake. Sikiliza alivyozung’mza na Mfalme Daudi kuhusu mwanae Sulemani atakayeketi kwenye kiti chake cha enzi juu ya Israeli:
1 Mambo ya Nyakati 22:9 Tazama, atazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe; nami nitamstarehesha mbele ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake.
Ile ahadi ya amani, kwa taifa ambalo lilipitia mapigano mengi, kwa Mfalme kama Daudi, aliyekuwa mpiganaji shujaa hata kabla ya kusimikwa kuwa mfalme …. kwa kweli ilikuwa ahadi ambayo ingewawia vigumu kuikubali mara moja.
Lakini usidanganyike hata kidogo. Mungu huyu anayekupenda kuliko jinsi ungeelezea, anataka kukukirimia amani yake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.