... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ahadi ya Kweli

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ezekieli 36:25-27 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

Listen to the radio broadcast of

Ahadi ya Kweli

Download audio file

Dhana ya kusalimisha maisha kwa Mungu na kuamua kumwishia na kumtii, ni dhana inayochukiza watu wengi.  Kwa nini, siku hizi za maendeleo, mtu angetaka kufanya hivyo?

Jessica, binti wa rafiki yangu wa karibu, aliolewa.  Moyo wangu ulijaa furaha wakati nilishuhudia wana arusi hawa wawili kuweka nadhiri ya kuishi pamoja.  Wengine wangeuliza, kwa nini siku hizi za maendeleo, watu wangetaka kufanya hivyo?

Na ndivyo ilivyo wakati sisi tunaipa kisogo dunia hii na kuweka nadhiri kwamba tutampenda Mungu peke yake, Mungu aliyetupenda kipeo, hata akakubali kumtuma Yesu, ili ateswe na kufa kwa ajili yetu.  Kwa mtazamo wake Mungu, inaonekana hivi:

Ezekieli 36:25-27  Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.  Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.  Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.

Na katika uhusiano huu wa karibu unaopendeza sana, katikati ya mipaka hiyo, mtu ataweza kutimiziwa kabisa, apate uhuru ambao hauwezi kupatikana po pote pengine. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy