Ahadi Zilizodhaminiwa
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Zaburi 138:2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, nitalishukuru jina lako, kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza ahadi yako, kuliko jina lako lote.
Nina swali kwako, je!, Unaweza kuamini ahadi za Mungu? Kuziamini kweli kweli pamoja na misukosuko tuliyonayo hapa duniani?, je! Bado ahadi za Mungu zinasimama pale pale, au labda zimeyumba na kuwa kama hadithi tu?
Unaona, ni vigumu kweli, sindiyo? mtu anapopitia kwenye kipindi kigumu, sio rahisi yeye kusimama kwenye ahadi za Mungu. Pale mazingira, watu na maisha kwa ujumla vinaenda kinyume na wewe, sio rahisi kujua kwenye kiini cha moyo wako kwamba ahadi zake ni hakika; kwamba atakuvusha salama na hatimaye mambo yatakuwa shwari.
Napenda sana Zaburi, ni kwasababu nyingi ziliandikwa na Mfalme Daudi akiwa anaangalia jinsi alivyokuwa kwenye hatari kubwa na kutafakari sehemu kubwa ambayo Mungu alikuwa nao kwa kumwokoa. Kwahiyo, sikiliza ufupisho wa mtazamo wa Daudi:
Zaburi 138:2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, nitalishukuru jina lako, kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza ahadi yako, kuliko jina lako lote.
Kwa sababu Mungu ni Mungu, jina lake lina maana sana; sifa zake pia ni muhimu kuliko vyote. Kwahiyo, Mungu anapotia jina lake kuthibitisha na kudhamini jambo fulani, basi litakuwa limetegemezwa kabisa! Kwahiyo, ni dhahiri kwamba Daudi alikuwa na shukrani kubwa kwa Mungu kwa kuwa alimwokoa mara nyingi, lakini pia alielewa malengo na makusudi ya Mungu kwa kumpitisha kwenye vipindi vigumu.
Mungu alikuwa anatimiza makusudi yake. Kwa kumwokoa mfalme aliyeteuliwa kuongoza Israel, taifa lake teule, Mungu alikuwa analitukuza jina lake katikati ya mataifa.
Tunawezaje kuwa na uhakika kwamba ahadi za Mungu ni za kweli? Ni kwa sababu zimedhaminiwa na Jina lake pamoja na Neno lake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.