Amani na Maangamizo
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 26:3-6 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa mllele. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, mji ule ulioinuka, aushusha, aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini. Mguu utaukanyaga chini, naam, miguu yao walio maskini, na hatua zao walio wahitaji.
Kuna hoja kubwa inayotumiwa na wanaopinga uwepo wa Mungu Mwenyezi, Mungu wa Upendo. Wanaileta hivi, “Kwanini Mungu anaruhusu mateso yaendelee kuwepo duniani? Ni wazi kwamba Mungu hatupendi kiasi cha kutokutaka kustopisha mateso yetu, au hana uwezo kuyathibiti.
Mtu akiiangalia kwa juujuu hoja hiyo inaonekana kama nikweli. Je! Mungu wa upendo anawezaje kuruhusu watu kuendelea kuteseka? Isitoshe, huyu Mungu wanayemsema kwamba ni wa upendo atakuja kuhukumu baadhi yetu na kututesa milele na milele katika moto wa Jehanamu?
Lakini chunguza vizuri mazingira ya uovu uliopo ulimwenguni, uovu uliotokana na maamzi huru ya Mungu aliyompa kila mwandamu hapo ndipo utakapoelewa upendo wa Mungu na hukumu zake, vyote vinaeleweka vizuri sana.
Isaya 26:3-6 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa mllele. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, mji ule ulioinuka, aushusha, aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini. Mguu utaukanyaga chini, naam, miguu yao walio maskini, na hatua zao walio wahitaji.
Kama Mungu ni Mungu kweli kweli, basi Yupo kwaajili ya kuwapa amani watu wanaomtumaini na usalama kwa wale wanamtegemea. Lakini pia, ataleta uharibifu na hukumu kwa wenye kiburi, kwa wao wanaowakandamiza maskini. Kazi zao zote zenye fahari atazibomoa ili maskini na wanyenyekevu waweze kuzikanyaga-kanyaga.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.